Wanafunzi zaidi ya 200 watekwa Nigeria

WANAFUNZI zaidi 200 nchini Nigeria wametekwa na watu wenye silaha katika mji uliopo Kaskazini wa Kuriga.

Idadi ya waliotekwa kutoka shule ya sekondari kulingana na takwimu tulizochukuwa ni 187, huku shule ya msingi ni 40 kwa sasa,” alisema mwalimu wa shule hiyo.

Diwani wa mtaa wa Kuriga Idris Maiallura alisema aliwahi kufika shuleni hapo na kuona watu hao wakiwa na wanafunzi 100 wa shule ya msingi lakini baadaye waliwaachia na wengine kutoroka.

Advertisement

Wazazi na wakazi walilaumu utekaji nyara huo kwa ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Gavana wa jimbo la Kaduna Uba Sani alitembelea Kuriga na kuahidi kuwanusuru wanafunzi hao, ofisi yake ilisema, lakini hakusema ni wanafunzi wangapi waliopotea.