FILAMU ya royal tour imeanza kuonesha mfanikio nchini, ambapo waandishi wa habari wa kimataifa 24 kutoka nje ya nchi watatembelea hifadhi ambazo hazijatangazwa ili zifahamike kimataifa na kuendelea kuifungua Tanzania.
Waandishi hao wataweza kuandika madhari mazuri ya Tanzania na vivutio vyote watakavyotembelea nchini,jambo litakaloongeza wigo wa watalii kuingia nchini.
Akizungumza jana Dar es Salaam , mratibu wa tukio hilo kutoka program ya Awoke International Sports Tourism and Expo, Buchebuche Enosy amesema kupitia filamu ya royal tour sekta ya utalii imefufuka na wanapokea watalii wengi kuliko kipindi chochote.
Amesema baadhi ya nchi ambazo waandishi hao watatoka ni pamoja na Marekani, Canada ,India, Uturuki, Israel na hata Ghana.
Buchebuche amesema ujio wa wandishi hao utasaidia kuona na kuandika pamoja na kutangaza nchi kupitia vyombo vya habari wanavyotoka .
“Tumeona jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais wetu katika kuifungua sekta ya utalii ambapo kupitia filamu ya royal tour sekta imefufuka na tunapokea wtalii wengi kuliko ilivyokula awali,”amesema na kuongeza kuwa waandishi hao wataingia nchini kuanzia mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
Amesema waandishi hao watatembelea mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro, Iringa, Njombe, Lindi, Mbeya, Rukea, Kigoma, Kagera, Geita, Mara,Pemba na Zanzibar.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Program hiyo, Ernest Mwakasenga amesema ziara ya wandishi hao wa Habari inaambatana na kuzindua program hiyo ya Awoke yenye malengo ya kuwaleta pamoja viongozi wa utalii na michezo nchini na kutengeneza muunganiko kwenye utalii.
Amesema uzinduzi huo utafanyika rasmi machi 27, mwaka huu Dar es Salaam na wageni 300 wanatrajiwa kushiriki.
Amesema yapo manufaa ya program hiyo ikiwa ni kuongeza idadi ya watalii nchini, kuongeza mapato Kwa serikalipamoja na jamii pamoja na kuifungua fursa mbalimbali.