Wanahabari wapatiwa elimu usimamizi wa maadili

WAANDISHI wa habari wanawake zaidi ya 116 wamepata mafunzo ya menejimenti ikiwemo usimamizi wa maadili na ushirikiano kwenye vyombo vya habari Tanzania Bara na Visiwani.
Akifungua mafunzo ya siku tatu yanayofanyika jijini Arusha na kushirikisha waandishi wa habari wanawake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzani (MCT), Kajubi Mukajanga amesititiza wanahabari wanawake wanapaswa kuwa viongozi wenye maamuzi ya kusimamia vyema maadili ya vyombo vya habari.
“Waandishi wa habari wanawake ni viongozi wazuri endapo vyumba vyao vya habari vikiwapa nafasi pasipo kubaguliwa ingawa tunajua vyombo vingi vya habari vinaongozwa na wanaume lakini tunasisitiza pia wanawake wanahabari wapate nafasi za uongozi.” Amesema Mukajanga
Naye mmoja kati ya wakufunzi mkongwe katika tasnia ya habari, Pili Mtambalike amesema uongozi bora ni ushirikiano baina ya waandishi wa chini na wahariri katika kuhakikisha kazi zinazofanywa zinafanyika kwa usahihi sanjari na mabosi kuthamini kazi zinazofanywa na wanahabari kwa kuwashukuru.
Ameongeza pia ni lazima wanahabari wanawake wakawa wabunifu katika uboreshaji wa kazi zao wanazosimamia ikiwemo kujali maslahi ya wanahabari wengine wanaowaongoza na kutambua mchango wa kila mtu katika tasnia ya habari pamoja na kugatua madaraka ili hata mhusika atakapoondoka kunamtu anaweza kusimamia kazi mbalimbali ili ziende.
MCT imetoa mafunzo ya wanahabari wanawake katika masuala ya uongozi ikiwemo rasilimali fedha na sheria mbalimbali tangu mwaka 2019 na wanahari mbalimbali wamenufaika katika mikoa ya Morogoro,Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Moshi na sasa Mkoa wa Arusha.
[๐๐จ๐ฐ ๐๐จ ๐๐๐ค๐ ๐๐ฑ๐ญ๐ซ๐ ๐๐ง๐๐จ๐ฆ๐ ๐ ๐ซ๐จ๐ฆ ๐๐จ๐ฆ๐ ๐๐ก๐๐ง๐ ๐ ๐๐จ๐ฎ๐ซ ๐๐ข๐๐ ๐๐๐]ๅฝกโ
๐๐จ๐จ๐ ๐ฅ๐ ๐ข๐ฌ ๐ฉ๐ซ๐๐ฌ๐๐ง๐ญ๐ฅ๐ฒ ๐ฉ๐๐ฒ๐ข๐ง๐ $๐๐,๐๐๐ ๐ญ๐จ $๐๐,๐๐๐ ๐๐ฏ๐๐ซ๐ฒ ๐ฆ๐จ๐ง๐ญ๐ก ๐๐จ๐ซ ๐ฐ๐จ๐ซ๐ค๐ข๐ง๐ ๐จ๐ง ๐ญ๐ก๐ ๐ฐ๐๐ ๐๐ซ๐จ๐ฆ ๐ก๐จ๐ฆ๐. ๐ ๐ก๐๐ฏ๐ ๐ฃ๐จ๐ข๐ง๐๐ ๐ญ๐ก๐ข๐ฌ ๐๐๐ญ๐ข๐ฏ๐ข๐ญ๐ฒ ๐ ๐ฆ๐จ๐ง๐ญ๐ก๐ฌ ๐๐๐๐ค ๐๐ง๐ ๐ ๐ก๐๐ฏ๐ ๐๐๐ซ๐ง๐๐ $๐๐,๐๐๐ ๐ข๐ง ๐ฆ๐ฒ ๐๐ข๐ซ๐ฌ๐ญ ๐ฆ๐จ๐ง๐ญ๐ก ๐๐ซ๐จ๐ฆ ๐ญ๐ก๐ข๐ฌ ๐๐๐ญ๐ข๐ฏ๐ข๐ญ๐ฒ. ๐ ๐๐๐ง ๐ฌ๐๐ฒ ๐ฆ๐ฒ ๐ฅ๐ข๐๐ ๐ข๐ฌ ๐ข๐ฆ๐ฉ๐ซ๐จ๐ฏ๐๐ ๐ญ๐จ๐ญ๐๐ฅ๐ฅ๐ฒ!
.
.
๐๐จ๐จ๐ค ๐๐ญ ๐ข๐ญ ๐ฐ๐ก๐๐ญ ๐ ๐๐จ—————————->> http://www.join.hiring9.com