Wanahabari wapewa somo uwasilishaji taarifa

WAANDISHI wa habari kutoka Lindi na Mtwara wameaswa kuepuka uposhaji wa makusudi wanapowasilishwa takwimu pamoja na taarifa wanazozipeleka kwa Wananchi.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kutokana na nafasi kubwa waliyokuna nayo wanahabari hao hivyo ni lazima waipatie heshima tasnia hiyo.

Kanali Abbas amezungumza hayo katika mafunzo ya siku mbili yanayoendelea kwa wanachama wa klabu za waandishi wa habari wa mikoa hiyo kuhusu usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanayofanyika mkoani Mtwara,

Mafunzo hayo yanayofanyika leo, RC Abbas amesema wanapotekeleza majukumu yao hayo pia wajiepushe na kutumika na baadhi yao  kwa kuwafanya wakubalike au wawe na mvuto katika maeneo yao ya kiutawala kwa kuripoti tu yale ambayo wao wangetamani wayaripoti kwa ajili yao na kupelekea kuwajengea umaarufu.

‘’Jielekezeni kwenye uandishi wa habari unaolenga kutatua kero au migogoro badala ya kuikuza na daima hakikisheni kazi zenu zinatoa majibu ya kero za wananchi badala ya kuacha maswali na kila unapomaliza kuandika habari yako jiulize inasaidia vipi jamii kutatua kero inayowakabili au itakuwa na madhara gani kwa jamii, serikali au  kwa usalama wa taifa’’amesema Abbas

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022,  Anne Makinda  mewapongeza wanahabari hao kwa jitihada zao kubwa za kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini na mafunzo hayo  ni moja ya ushirikishwaji wa utekelezaji wa zoezi hilo kwasababu ni jambo endelevu.

‘’Kwahiyo hiki tunachokifanya ni utekelezaji wa mwongozo ule tungependa waandishi wa habari kila katika akili zao, mipango yao, kazi zao wajue kuna kitu kama hicho, wanaweza kudadisi na kuuliza maswali, hapa tumekusanyika siyo kongamano ni darasa na elimu haina mwisho kwahiyo wito wangu mkubwa kwenu hizi siku mbili ni dhahabu kwenu kwa kazi yenu’’amesema Makinda

Aidha kupitia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 mpaka sasa wameshatoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari zaidi ya 500 katika mikoa mbalimbali nchini kati yao wakiwemo 70 katoka mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara.

Zoezi hilo la mafunzo lilianza Julai 2023  kwa mikoa Ruvuma, Njombe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Shinyanga, Geita, Simiyu, Kagera, Mwanza, Mara, Arusha, Manyara, Lindi pamoja na Mtwara, zoezi ambalo ni endelevu kwa mikoa mingine nchini na mikoa ya Lindi na Mtwara ni kudi la sita kufanyika mafunzo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Tamali William amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo yanayoendeshwa na ofisi ya Taifa ya takwimu na ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali ya Zanzibar yanayofanyika kwa mujibu wa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Habari Zifananazo

Back to top button