BENKI ya Maendeleo imetangaza ongezeko la gawio kwa wanahisa ambalo ni sh milioni 708 kwa mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 136 ikilinganishwa na gawio la shilingi milioni 11 kwa mwaka 2021
Hayo yamesemwa leo Agosti 9,2023 na Mkuu wa Idara ya usimamizi wa hatari na taratibu wa benki hiyo Peter Tarimo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
Amesema, gawio hilo kwa wanahisa litalipwa Oktoba 6,Octoba 2023 kwa wanahisa wote watakaokuwa wamejisaji.
Aidha, amesema gawio hilo ni mgao wa nne tangu kuanzishwa kwa benki hiyo mwaka 2013 .