Wanajeshi 14 wafa kwa kipindupindu DR Congo

TAKRIBANI wanajeshi 14 wamekufa nchini DR Congo na wengine 500 wameathiriwa na mlipuko wa kipindupindu Kusini-Mashariki mwa Mkoa wa Haut-Katanga, jeshi limeeleza katika taarifa yao.

Jenerali Eddy Kapend, kamanda wa eneo la 22 la kijeshi, kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Mura, alithibitisha vifo hivyo wakati wa mkutano na ujumbe kutoka ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) mjini Lubumbashi.

“Kufikia saa 72 zilizopita, idadi ya wagonjwa wanaopokea matibabu iliongezeka hadi 144 haswa. Tumerekodi vifo 14 na tumeokoa wagonjwa wengi ambao wamerejea katika viwango vyao”. Jenerali Kapend alisema.

Alisema mlipuko huo ulisababishwa na hali mbaya katika kambi ya kijeshi.

Habari Zifananazo

Back to top button