Wanajiolojia kukutana Zanzibar kujadili uchumi wa buluu

ZANZIBAR ZAIDI ya wanajiolojia 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kukutana Zanzibar kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mchango wa tasnia yao katika uchumi wa buluu.

Akizungumza na vyombo vya habari Visiwani humo leo, Ijumaa, Rais wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania, Dr Elisante Mshiu amesema kuwa mkutano huo utafanyika Mjini Unguja Novemba 7-11, mwaka huu, ambapo mada kadha wa kadha zitajadiliwa ikiwemo uchumi wa buluu.

“Maandalizi ya mkutano kwa ujumla yanaendelea vizuri na tayari hatua kubwa imepigwa. Niseme kwa ufupi tu kuwa mkutano wa mwaka huu sio wa kukosa na ni fursa adhimu kwa wanajosayansi kuelewa kwa mapana dhana nzima ya uchumi wa buluu na nafasi ya kada hii katika kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya dhana hii,” Dr Mshiu amesema.

Mkutano utakwenda sanjari na maonesho ya bidhaa na huduma kutoka kampuni mbalimbali na washiriki kutembelea maeneo ya kijiolojia na kitalii yaliyopo Zanzibar.

pharmacy

Habari Zifananazo

Back to top button