Wanamgambo 10 wauawa katika shambulio Niger

WANAJESHI wanane wamejeruhiwa na wanamgambo 10 kuuawa katika shambulio lililohusisha silaha Kaskazini mwa Niger.

Takriban wanamgambo 10 waliuawa na wanajeshi wanane kujeruhiwa wakati wa shambulio lililotekelezwa na kundi lenye silaha katika eneo la Agadez kaskazini mwa Niger.

Shambulio hilo pia lilisababisha kujeruhiwa kwa raia mmoja, na kukamatwa kwa mtu aliyekuwa na bunduki, Wizara ya Ulinzi ya Nigeria ilisema, na kuongeza: “Wapiganaji hao walilenga wakati wa shambulio lao kikosi cha Wanajeshi wa Nigeria waliokuwa wakilinda.”

Wizara hiyo imethibitisha katika taarifa yake kwamba wanajeshi hao wa Nigeria waliweza kuzima shambulio hilo na kuharibu magari kadhaa, bunduki za rashasha, makombora, bunduki za kivita, na kiasi kikubwa cha risasi pia walikamatwa, pamoja na baadhi ya nguo za kijeshi.

Habari Zifananazo

Back to top button