Wananchi Chad waunga mkono katiba mpya

WANANCHI wa Chad wamepiga kura kuunga mkono katiba mpya ambayo wakosoaji wanasema itampa nguvu ya kimamlaka ya kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby.
Kura ya maoni iliyofanyika mapema mwezi huu iliidhinishwa na asilimia 86 ya wapiga kura, tume ya serikali iliyoiandaa ilisema jana huku idadi ya wapiga kura ilikuwa asilimia 64%.
Viongozi wa kijeshi wa Chad wameitaja kura hiyo kuwa hatua muhimu kuelekea uchaguzi mwaka ujao kurejea kwa muda mrefu katika utawala wa kidemokrasia baada ya kuchukua mamlaka mwaka 2021 wakati rais wa zamani Idriss Deby aliuawa uwanja wa vita wakati wa vita na waasi.
Katiba mpya itadumisha serikali ya umoja, ambayo Chad imekuwa nayo tangu uhuru, wakati baadhi ya wapinzani wake walitaka kuundwa kwa serikali ya shirikisho, wakisema itasaidia kuchochea maendeleo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button