Wananchi Kusini washauriwa kutumia mazao ya lishe

WANANCHI wa Kanda za Juu Kusini, wameshauriwa kutumia mazao yenye viini lishe ili kujikinga na udumavu unaowaathiri watoto kwa kiwango kikubwa katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI), Kituo cha Uyole mkoai Mbeya, Dk Denis Tippe ameeleza hayo alipozungumza na HabariLeo kuhusu utafiti wanaoufanya kuhusiana na mazao lishe mbalimbali yakiwemo maharage ya Jesca.

Amesema pamoja na ukweli kuwa, ukanda huo ni kapu la chakula, bado kuna changamoto kubwa ya udumavu hadi kufikia asilimia 35 hadi 40.

Amesema kutokana na sababu hiyo wamekuwa wakitangaza maharage aina ya Jesca ambayo yana virutubisho vingi ikiwemo zinki na madini ya chucma ambayo inahitajika zaidi katika ukuaji na lishe kwa ujumla.

“Hivyo maharage kama Jesca kwa sababu ya virutubisho vilivyopo tunazidi kuyatangaza ili watumiaji, wakulima na walaji waweze kutumia,” amesema.

Pia alisema kituo cha Uyole kina mazao mbalimbali likiwemo la ulezi ambalo linafanyiwa utafiti, na tayari kuna mbegu aina tatu zimeshatolewa na nyingine sita zipo kwenye hatua ya mwisho.

” Tunapozungumzia lishe tunazungumzia katika kuboresha mifupa kwa ajili ya calcium iliyoko katika zao la ulezi,” amesema

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button