Wananchi Mbarali kupiga kura kesho
MBEYA,Mbarali: Wananchi wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya kesho wanatarajia kupiga kura kumchagua Mbunge.
–
Uchaguzi huo unafanyika kuziba nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega ambaye alifariki Julai mosi mwaka huu kwa ajali ya kugongwa na trekta dogo maarufu Power Tiller wakati akiendesha pikipiki kuelekea shambani kwake.
–
Agosti 5 mwaka huu, Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ilitangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mdgo katika Jimbo la Mbarali, na kata sita katika mikoa tofauti.
–
Baada ya tangazo hilo mchakato wa kuwapata wagombea ulifanyika ndani ya vyama na wagombea kutoka vyama 14 vya siasa nchini walijitokeza kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Mbarali.
–
Vyama vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo ni pamoja na chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Labor Party (TLP), United Democratic party (UDP), ACT Wazalendo, Democratic Party (DP), Alliance for African Farmers party (AAFP), Chama cha Kijamii (CCK) Alliance for Democratic Change (ADC), NLD, NRA, UMD, ADA -TADEA na Chama cha Demokrasia Makini.
–
Septemba 10, mwaka huu kampeni za uchaguzi huo zilizunduliwa huku wagombea kutoka vyama shiriki wakijinadi kwa waanchi amabapo changamoto zilizopo kwenye kilimo, pamoja na Miundombinu zilizungumziwa na wagombea huku wakiahidi kuzitatua.
–
Aidha kesho uchaguzi unatarajiwa kufanyika katika kata sita kuchagua madiwani ambazo ni Nala Dodoma,Old Moshi Magharibi,pamoja na kata ya Kitowo iliyopo Rombo.
–
Nyingine ni Mtyangimbole iliyopo Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Manispaa ya Songea.