Wananchi Mtwara watakiwa kuendeleza urithi wa Nyangumi

WANANCHI mkoani Mtwara wametakiwa kuuendeleza kuona urithi wa Nyangumi uliyopo katika Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ikiwa ni sehemu muhimu kwao na ustawi wa mkoa huo kwa ujumla.

Akizungumza wiki hii katika uzinduzi rasmi wa msimu wa Nyangumi uliyofanyika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na maingilio ya Mto Ruvuma iliyopo kata ya Msimbati Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema wanayo kila sababu ya kujivunia urithi huo.

‘’Sisi mtwara tuna kila sababu ya kujivunia kutokana Nyangumi kuona ipo sababu ya kuja kwenye maeneo ya Mtwara zaidi kuliko maeneo mengine ya maji kwahiyo tunazo kila sababau ya kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa urithi huu kwahiyo nitoe rai tujitahidi kuona urithi huu ni sehemu muhimu kwa ustawi wa Mkoa wa Mtwara na tuone kila sababau ya kuuendeleza.” amesema Abbas.

Advertisement

Aidha wanyama hao kila mwaka husafiri kutoka Pwani ya Kusini kuja Pwani ya Kaskazini au Kusini zaidi kwasababu kipindi hiki ni cha joto wakati wanakotoka ni kipindi cha baridi pia ni mnyama anayeweza kusoma mazingira yenye utulivu na salama kwake na kuyakariri hivyo hizo ni sababau za msingi kwake zinazopelekea kila mwaka kuweza kuonekana katika maeneo hayo ya Msimbati.

Wanyama hao wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali ikiwemo kuvuliwa, kunasa kwenye nyavu kwa bahati mbaya na wakati mwingine kujeruhiwa na meli zinazotembea baharini ambapo asilimia 71 ya eneo la ardhi ni la maji hivyo Shirika la Kimataifa la Uhifadhi limeweka kwenye kundi la viumbe waliyoko hatarini kutoweka.

Mhifadhi mfawidhi wa hifadhi hiyo, Redfred Ngowo  amesema tukio hilo ni mara ya kwanza kufanyika na la kihistoria kwao na eneo hilo ni bora kwa kuwatazama viumbe hao, kulitumia kwa ajili ya utalii na ni eneo ambalo viumbe hao wanakuja kwa ajili ya kuzaliana hivyo linatoa fursa kubwa kuweza na kuboresha utalii mkaoni humo, kauli mbiu yao mwaka 2023 inasema ‘Tembelea wekeza tuendeleze Mtwara yetu’ ambapo mwaka 2022 idadi ya wageni waliyotembelea hifadhi hiyo 560,  na mwaka 2023  ni 630.

Ofisa utalii mkoani humo, Juvenari Jakamwambi  ameendelea kusistiza kuwa wananchi hao kuja kuangalia kivutio hicho ambacho adimu kuwaona mahali pengine utalii ambao unapatikana pwani hiyo kuanzia Julai hadi Novemba kila mwaka jambo ambalo linapaswa kupongezwa na sasa watalii wengi wanakuja kwenye eneo hilo na huduma zipo za kutosha.

Diwani wa kata hiyo, Rashidi Omari ‘’Sisi wananchi wa naeneo  haya tunashikuru kuwepo kwa utali huu ambao utaenda kutunufaisha wanamtwara kwahiyo ni fursa kubwa kwetu kwasababu uchumi utaongezeaka hivyo tunaishukuru sana serikali kwa kuendeleza sekta hii na tunawahamasisha hata watu wengine ndani na nje ya nchi waje Mtwara fursa ya utalii ipo’’,amesema

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *