Wananchi Murriet waishukuru serikali huduma za jamii

Wananchi zaidi ya 800 wa kata ya Murriet jijini Arusha wamemshukuru serikali kupitia kwa Wakala wa Barabara za Vijijni na Mijini (TARURA) Mkoa wa Arusha kwa kutoa zaidi ya Sh milioni 199 kwaaajili ya utengenezaji wa barabara ya kituo cha afya Murriet hadi kwa Morombo kupitia Machwa.

Wakitoa pongezi hizo katika mahojian na mwandishi wa habari hii,wakazi hao akiwemo dereva wa bodaboda Jumanne Issa,Abraham Kambaga na Aziza Bakari wamesema kuwa barabara hiyo ilikuwa na mabonde na mashimo mashimo mengi na kuleta usumbufu kwa wananchi wa mtaa wa Mlimani hususan nyakati za mvua.

Bakari amesema barabara hiyo awali ilikuwa na changamoto kubwa ya mashimo mashimo na kuepelekea magari kuharibika na wanafunzi kushindwa kwenda shule kwa wakati hususan nyakati za mvua

Naye Diwani wa Kata hiyo,Francis Mbise amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha zaidi ya sh,milioni 199 kupitia Tarura ili kutengeneza barabara ya Machwa ambayo ni muhimu kwa kata hiyo na kata za jirani za Sombetini,na wananchi wanaokwenda eneo la Mirongo wanaitumia kwaajili ya usafiri

“Tunamshukuru Rais kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha changarawe tunaomba tuweke lami ili barabara hii iweze kupitika kwa saa zote”

Kutengenezwa kwa barabara hiyo kuondoa malalamiko ya wananchi ambao wanatumia barabara hiyo iliyokuwa na mashimo na na kuharibu magari ikiwemo wanafunzi kuanguka sababu ya matope kutokana na utelezi nyakati za mvua.

Habari Zifananazo

Back to top button