Wananchi wachekelea kilichofanywa na TRA katika Zahanati
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya mapato Tanzania Mkoa wa Kodi Temeke imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni nane kwenye Zahanati ya Mji mwema Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hayo ameyasema Meneja msaidizi wa huduma TRA Temeke, Edson Isanya wakati wakikabidhi msaada huo Desemba 2,2023.
Amevitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda viwili, mashine moja ya kupimia mapigo ya moyo,magodoro 20, mashuka 60, vitanda viwili vya kujifungulia pamoja na baiskeli mwendo mbili.
Aidha ameongezea kwa kusema wameamua kushirikiana na jamii ili waweze kurudisha kidogo walichokipata.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi Zahanati ya Mji mwema, Amani Leguna ameshukuru kwa msaada huo na ameongezea kwa kusema Zahanati hiyo ilikuwa inakumbwa na changamoto ya vitanda vya kujifungulia na kwa siku walikuwa wanapata wagonjwa wawili hadi watatu hivyo itasaidia kupunguza changamoto hiyo.
Nae Mwananchi wa Mji mwema, Salma Abdalah amesema msaada huo utachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwenye Zahanati hiyo