Wananchi wapewa mbinu kumaliza ukatili wa Kijinsia

PWANI; ZAIDI ya matukio 508 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa mwezi Julai 2022 mpaka Mei 2023, kwenye Wilaya ya kibiti mkoani Pwani ukatili huo ni wa kingono ,kimwili, jinsia na ukatili wa watoto

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Canal,Joseph Kolombo Novemba 28,2023 kwenye Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  kwa wanawake na watoto yaliyowakutanisha Wananchi wa wilaya hiyo pamoja na wadau mbalimbali

Maadhimisho hayo yameanza Novemba 25,2023 ambapo kilele chake Duniani mwaka huu yataadhimishwa Disemba 10, 2023

Advertisement

Kolombo  amesema ataunda kamati za jinsia kwenye wilaya hiyo ili kuboresha na kutatua ukatili wanaofanyiwa wananchi hao.

Kwa upande wake Jacob Kashinge Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Kibiti amesema wilaya hiyo inakumbwa na changamoto kubwa ya ukatili wa kingono ambapo unapelekea kesi nyingi za kingono kushamiri kwenye wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine , Agatha Lema  Ofisa miradi K.K.K.T Dayosisi ya Mashariki na Pwani ameongezea kwa kusema ushirikiano wananchi ni mdogo na kuwataka kubadilika na kuanza kushirikiana ili kutokomeza vitendo hivyo.

Baadhi ya wananchi walioshiriki maadhimisho hayo wamesema jukumu la kuwatunza na kuwalea watoto linaanza na wao wenyewe hivyo watahakikisha watatokomeza ukatili huo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni chanzo cha Umasikini ngazi ya familia na Taifa

 

 

2 comments

Comments are closed.