Wanaoenda kwa waganga kusaka utajiri waonywa

KIONGOZI wa kimila, jadi, asili na utamaduni kutoka himaya ya Nyarutambwe Manyovu mkoani Kigoma, Dk Fadhil Emil, amewataka vijana kwenda kwa waganga kuomba ushauri namna ya kufanya kazi kwa bidii na sio kutafuta utajiri.

Amesema ili kufikia mafanikio inahitajika uzalendo, kujituma na kujua wajibu wakitambua kuwa kupambana katika maisha ndiko ufanisi unakopatikana.

Amesema hayo leo Dar es Salaam, wakati viongozi wa mila na jadi walipokutana na vijana chini ya taasisi ya wafikiriaji duniani kwa lengo la kupanga na kutathmini namna ya kuwafikia viongozi wakuu wa nchi kwa lengo la kujifunza kuhusu usimamiaji wa maadili.

Advertisement

Amesema licha ya kwamba yeye ni mganga, daktari na kiongozi wa kijadi, lakini amepambana kwa kujiendeleza kusoma katika nchi mbalimbali, ili kuwezesha ndoto zake za kuwa na maisha mazuri kufikiwa.

“Mimi ni mganga, huwa napokea watu wengi wakiwemo vijana wakitaka kupata utajiri na wengi wanapoulizwa wanajihusisha na nini, hudhani kuwa waganga tunataka kuwatoza fedha kumbe lengo ni kutaka kujua unachofanya ili ushauriwe kwenye eneo hilo,” amesema.

Amesema vijana hawajui jitihada alizofanya katika kusoma akiwa, ametembelea nchi 165, mabara manne akiendelea kupambana, ili aishi vizuri na anayaishi hivyo vijana wasihangaike kwenda kwenye maombi ama kwenda kwa waganga ili kupata utajiri.

Amesema wakati mwingine waende kwa waganga kwa ajili kushauriwa namna ya kufanikiwa, kwani wapo wanaodhani kuwa mafanikio yanapatikana kirahisi.

Dk Fadhil amesema katika mafanikio kunahitaji uzalendo, kujituma na kila mmoja kujua wajibu wake huku akiwabeza wanaume wanaoshindwa kuwajibika kutimiza majukumu yao katika ndoa ama familia na kusababisha ndoa kusambaratika.

“Lazima kujitambua kuwa kama ni mwanaume , wajibika katika majukumu yakupasayo, ukikosa nenda kwa viongozi wa kimila kupata ushauri na sio maombi pekee bila kufanya kazi,” amesema.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *