Wanaoishi hifadhi ya Ngorongoro wana changamoto ya upumuaji

WANAOISHI ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto ya magonjwa ya upumuaji, kuharisha, magonjwa ya ngozi kutokana na hali halisi ya uchafu na moshi unatoka ndani ya maboma ya wafugaji.
Akiongea na waandishi wa habari katika Zahanati ya Oloirobi Tarafa ya Ngorongoro Kata ya Ngorongoro, Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Silvia Malloy amesema wagonjwa wengi wanaofika kupata matibabu wanatokana na magonjwa hayo matatu yanayosumbua zaidi.
Sababu kubwa ya magonjwa hayo yanachangiwa na hali halisi ya mazingira ya baridi na jamii hiyo kushindwa kujisitiri nyakati za baridi haswa ugonjwa wa niomonia na mazingira ya usafi wa chakula si mazuri pamoja na magonjwa ya ngozi sababu wanalala na mifugo kama mbwa ndani ya maboma yao
“Nyumba wanazoishi zinasababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji sababu wanakoka moto ndani yake na kulala na mifugo ndani lakini pia maboma yao hayana madirisha ya kutolewa hewa hali inayopelekea ndani kuwa na moshi mkubwa unaoleta madhara kwao”
Zahanati hiyo unahudumia vijiji vitatu ambavyo ni Oloirobi,Kayapus na Mokilal ambapo awali msanii Suleiman Msindi maarufu kwa jina la” Afande Sele” alitoa rai kwa wananchi hao kuhama kwa hiari kwani mazingira halisi ya maboma yao kwa baadhi ya jamii hiyo ya kifugaji si rafiki kutokana na kuishi na mifugo kama mbwa ndani ya boma sanjari na moshi mwingi usiokuwa na eneo la kutolewa hewa sababu wanapikia ndani lakini pia wanapata joto kubwa sababu ya hali halisi ya baridi iliyopo nje ya maboma yao