Wanaoivisha matunda kwa moshi wakemewa

WIZARA ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imekemea tabia ya baadhi ya wakulima kuchimba mahandaki na kuingiza mazao kwa ajili ya kuyaivisha kwa njia ya moshi na kuyapeleka sokoni.

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis alitoa karipio hilo jana akijibu swali la Mwakilishi wa Kiwani, Foum Mussa Foum (CCM), aliyetaka kufahamu wizara inavyokabiliana na tabia ya wakulima kuvuna mazao machanga na kuyaivisha kwa kuchimba handaki na kutumia moshi.

Akijibu swali hilo, Khamis alikiri kuwa mbinu hizo zinafahamika na alipiga marufuku kutumika tena.

Alisema mbinu hizo zilikuwa zikitumiwa na wazee katika miaka ya nyuma kuivisha mazao ndizi na maembe kabla ya kupelekwa sokoni.

Alisema utaratibu wa sasa ni mbaya zaidi kwa sababu wakulima wanavuna mazao ambayo hayajafikia ubora wa kuingizwa sokoni na kulazimisha yaive haraka.

Alisema wizara ipo katika hatua za mwisho za kutunga mwongozo wa kufuatwa wa kulinda mazao ya kilimo ya matunda, ikiwemo kuhakikisha yanaiva na kuwa tayari kuingizwa sokoni.

Alisema wizara tayari imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwamba wananunua bidhaa za matunda ambayo hayajafikia muda wake wa kuingiza sokoni na matokeo yake hukosa ladha.

Matunda yanayotumiwa na wakulima kuivishwa haraka kwa kuchimba mahandaki ni pamoja na maembe, ndizi pamoja na mafenesi.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button