Wanaojenga SGR wasaidia yatima

DAR ES SALAAM; KAMPUNI ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa nchini (SGR), imetoa msaada kwenye kituo cha Mama Mwana Orphanage Center kilichopo Vingunguti, Dar es Salaam wenye lengo la kurudisha fadhila kwa jamii

Ofisa Uhusiano wa kampuni kampuni ya Yapi Merkezi, Hamisa Juma akizungumza wakati akikabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam, amesema wanatoa msaada kwa jamii kutokana na sehemu kubwa ya miradi inapopita baadhi ya watu wengi wanakuwa wanaathirika wa mradi kwa namna mbalimbali.

Kwa upande wake mlezi wa kituo hicho, Saada Ally ameshukuru kwa msaada huo na kutoa wito kwa jamii kuwakumbuka wenye uhitaji.

Amesema wanakabiliwa na changamoto ya sehemu ya kukaa kwani wanalipia gharama kubwa nyumba pamoja na bima za afya kwa watoto.

Habari Zifananazo

Back to top button