Wanaojifungua Watoto Njiti kuongezewa muda wa likizo

ARUSHA: MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewataka waajiri nchini kuwapa muda zaidi wa likizo wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti ili kuhakikisha ustawi wa afya ya mama na mtoto.

Dk Mpango ametoa agizo hilo leo jijini Arusha, alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya kitaifa Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi 2024.

“Mfanyakazi atakapojifungua mtoto njiti, kipindi cha uangalizi hakitahesabiwa kuwa sehemu ya likizo yake ya uzazi,” ameelekeza kiongozi huyo

Aidha, amesema mzazi anapaswa kutoka kazini Saa 7:30 Mchana kila siku kwa muda wa miezi sita baada ya kujifungua ili apate muda zaidi wa kunyonyesha.

Katika hatua nyingine, Dk Mpango amewataka wafanyakazi nchini kusimama katika weledi na kuacha uzembe wawapo kazini.

“Kwa Wafanyakazi ambao hawatumii nafasi zao ipasavyo watumie siku hii kujitafakari,” ameasa kiongozi huyo.

Habari Zifananazo

Back to top button