Wanaopisha mradi wa Msimbazi kulipwa mwezi huu

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema wananchi wanaopisha mradi wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi mkoani Dar es Salaam wataanza kulipwa fidia mwezi huu.

Mratibu Msaidizi wa mradi huo, Nyariri Kimacha alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao cha utambulisho wa mtaalamu mshauri wa masuala ya fidia. “Serikali imeshakabidhi fedha za kulipa fidia.

Ndani ya mwezi huu wa kumi fedha hizo zitaanza kulipwa,” alisema Kimacha.

“Ikifika kesho jioni (leo) tutaandaa tangazo kutaarifu wananchi kuwa sasa zoezi hili la kupokea fidia limefika. Wananchi watajulishwa tarehe ni lini na wapi,” alisema mtaalamu wa masuala ya kijamii kutoka Tamisemi, Beatrice Mchome. Aliongeza:

“Tutakusanya taarifa ili zisaidie mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za watoto wa shule ili Tamisemi ione namna watoto hawa watakavyohamishwa shule bila usumbufu.” Mchome alisema walifanya mpango wa ardhi mbadala kwa watakaopenda kwenda katika maeneo ya Mvuti, Kigamboni na Tegeta.

“Kwa mara ya kwanza mradi mkubwa unatekelezeka mara moja zaidi ya watu 3,000 wanahama katika bonde hilo,” alisema.

Alieleza shida ya malalamiko kutoka kwa wananchi yalianza wakati yalipofanyika makosa ya kibinadamu na akasema serikali haiwezi kutekeleza mradi bila kuzingatia sheria ya nchi. OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema wananchi wanaopisha mradi wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi mkoani Dar es Salaam wataanza kulipwa fidia mwezi huu.

Mratibu Msaidizi wa mradi huo, Nyariri Kimacha alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kikao cha utambulisho wa mtaalamu mshauri wa masuala ya fidia. “Serikali imeshakabidhi fedha za kulipa fidia. Ndani ya mwezi huu wa kumi fedha hizo zitaanza kulipwa,” alisema Kimacha.

“Ikifika kesho jioni (leo) tutaandaa tangazo kutaarifu wananchi kuwa sasa zoezi hili la kupokea fidia limefika. Wananchi watajulishwa tarehe ni lini na wapi,” alisema mtaalamu wa masuala ya kijamii kutoka Tamisemi, Beatrice Mchome. Aliongeza:

“Tutakusanya taarifa ili zisaidie mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za watoto wa shule ili Tamisemi ione namna watoto hawa watakavyohamishwa shule bila usumbufu.” Mchome alisema walifanya mpango wa ardhi mbadala kwa watakaopenda kwenda katika maeneo ya Mvuti, Kigamboni na Tegeta.

“Kwa mara ya kwanza mradi mkubwa unatekelezeka mara moja zaidi ya watu 3,000 wanahama katika bonde hilo,” alisema. Alieleza shida ya malalamiko kutoka kwa wananchi yalianza wakati yalipofanyika makosa ya kibinadamu na akasema serikali haiwezi kutekeleza mradi bila kuzingatia sheria ya nchi.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button