Wanaosafirisha Mifugo nje ya nchi wapewa maelekezo

TABORA: Wafugaji na wafanyabiashara wote nchini wanaosafirisha mifugo kwenda nje ya nchi wametakiwa kuacha kununua mifugo katika Minada ya awali badala yake kwenda kununua kwenye ile ya Upili ili kuifanya sekta ya Mifugo kuwa kubwa na kuchangia pato la Taifa.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 14, 2023 na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua wakati akizungumza na wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Ndala uliopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Kamanda Pasua amesema kuwa, kwenye minada ya awali havitolewi vibali vya kusafirisha mifugo kwenda nje ya nchi, hivyo waende kwenye minada ya Upili ama ya mpakani ambayo ni mikubwa na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo wanapatikana huko kwa ajili ya kuvitoa.

Aidha amesema Jeshi hilo linaendelea kutoa elimu katika minada yote nchini na kubainisha kuwa kupitia elimu hizo pamoja na mambo mengine wafugaji wanaelimishwa namna bora ya kufanya biashara bila kununua mifugo ya wizi ama ile yenye migogoro.

ACP Pasua amebainisha kuwa kwa wale ambao watabainika kusafirisha mifugo hiyo bila kufuata utaratibu kwa kukwepa kulipa ushuru ama kutokuwa na vibali, Jeshi hilo litachukua hatua za kisheria dhidi yao ikiwemo kukamata mifugo hiyo na kuwafikisha wahusika Mahakamani.

Kwa upande wake bwana Methew Kabundala kwa niaba ya Wafugaji amebainisha kuwa tatizo linalowakabili katika mnada huo ni mifugo kuwa mingi zaidi ya miundombinu ya mazizi hali inayopelekea biashara kufanyika nje, Hivyo akaiomba Serikali kuboresha mnada huo ili uweze kukidhi mahitaji.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

I am making $100 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning $16,000 a month by working on a laptop, that was really dumbfounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this for this job now by just using

this site link… http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
AmberRuiz
AmberRuiz
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by AmberRuiz
CandidaDorean
CandidaDorean
1 month ago

★ I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.( a02w)
Just open the link══════►►► http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x