Wanaowania Tuzo za Muziki watajwa

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk Pindi Chana ametangaza vipengele vya wanamuziki wanaowania tuzo za muziki mwaka 2023.

Dk chana ametangaza vipengele hivyo leo aprili 2023 jijini dodoma ambapo amevitaja baadhi kuwa ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike na wimbo bora wa mwaka ambapo amesema vipengele vingine vitaendelea kutangaza.

Katika kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume wanaowania ni Alli Kiba, Harmonize, Marioo, Rayvanny na Dullar Makabila.

Kipengele cha msanii bora wa kike wanaowania ni Nandy, Zuchu, Chemical Trixy Tonic na Waddy B.

Aidha ametaja kipengele cha wimbo bora wa mwaka ambapo zinazoshindanishwa ni Pita Huku wa Dullah Makabila, Nakupenda wa Jay Melody, Nitaubeba wa Harmonize, Kwikwi wa Zuchu pamoja na Mwamba wa Rayvanny.

Hata hivyo Dk Chana ameeleza kuwa, vipengele vya kuwania tuzo hizo vimeongezeka kutoka 47 hadi 57,huku akibaibisha kuwa zoezi la kuwapigia kura litaanza aprili 8, hadi 28, 2023 saa sita usiku na tuzo zitafanyika aprili 29, 2023 jijini dar es salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button