Wanasaini mkataba haki za kisheria kwa wanawake

SHIRIKA la Msaada ya Kisheria la Legal Services Facility (LSF) na Enabel na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji, yamesaini mkataba wa ruzuku wa Sh bilioni 10.

7 kutekeleza upatikanaji wa haki kwa wanawake kupitia msaada wa kisheria.

Makubaliano hayo LSF na Enabel zitashirikiana kuweka mazingira wezeshi na mazuri ya upatikanaji wa haki kwa kujenga uwezo wa wasaidizi

Advertisement

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema mradi huo shirikishi unafadhiliwa na umoja wa Ulaya chini ya mradi unaoitwa “Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling” na unalenga kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza usawa katika upatikanaji wa haki hususani kwa wanawake na wasichana.

Amesema kupitia mradi huo, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki.

“Tuna furaha kutia saini mkataba huu na Enabel, kwa kuwa umelenga katika kufikia malengo na hatua zote muhimu katika kuboresha upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria hasa kwa wanawake, wasichana, na jamii zote zilizopo nchini Tanzania”.

“Mradi huu, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki. Lulu amefafanua zaidi kuwa mradi huu utaongeza uelewa wa jamii hususani wanawake na wasichana kuhusina na umhimu wa msaada wa kisheria” amesema Ng’wanakilala

Mwakilishi mkazi wa Enabel nchini Tanzania, Koenraad Goekint, alisema ushirikiano huo unathibitisha dhamira yao ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria.

Ushirikiano huu unathibitisha dhamira yetu ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria”

Kwa upande wake Balozi wa Jumuiya ya Ulaya nchini Tanzania na Afrika Mashariki Christine Grau alisema kupitia mradi huo EU inaendelea kushirikiana na wadau katika kuongeza upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana hasa wale amabo ni whanga wa ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia.