Wanaswa kwa kukwepa pango la ardhi

WAMILIKI 42 wa ardhi mkoani Geita wamefikishwa kwenye vyombo vya dola ikiwemo katika mabaraza ya ardhi baada ya kubainika kuwa wadaiwa sugu waliokwepa kulipa pango kwa muda mrefu.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Geita, Rugambwa Banyikile ametoa taarifa hiyo leo mbele ya waandishi wa habari na kueleza hatua hiyo ni matokeo ya oparesheni maalumu iliyofanywa na maofisa ardhi.

Amesema kati yao, watuhumiwa 15 wameonyesha utayari wa kulipa deni la pango la ardhi huku taratibu za kisheria zikiendelea kuhakikisha wengine waliosalia wanatekeleza wajibu huo kwa mjibu wa sheria.

Aidha, amewaonya maofisa urasimishaji wa ardhi mkoani Geita kutokuwa chachu ya migogoro badala yake waendeshe mchakato huo kwa uhuru na uwazi ili hati za ardhi zitolewe kwa watu sahihi.

“Wananchi wanaopakana wote wawepo eneo husika, na ziwepo fomu maalum za kusaini na kukubaliana kwamba huu ndi mpaka wetu ili leo na kesho tusije tena tukapata malalamiko ya muingiliano wa ardhi.

Amekemea tabia ya maofisa wa ardhi kutohudumia wananchi kwa wakati kwani ucheleweshaji wa hati miliki za aridhi zinakwamisha maendeleo ya wananchi kushindwa kutumia ardhi yao kwa tija.

“Nitoe rai kwa maofisa aridhi wa halmashauri zote kuhakikisha kwamba kila mwananchi aliyelipia gharama za umilikishaji ndani ya siku mbili hati yake iwe imekwishaandaliwa.

“Pia kuhakikisha kwamba inafikishwa ofisi ya kamishina wa ardhi kwa ajili ya kusainiwa na kusajiliwa na msajili msaidizi wa hati wa mkoa.

” Aliagiza na kusisitiza;

“Ni vizuri kabisa tuhakikishe kwamba haki za watu zinatendeka kwani sisi ni kama mamlaka wezeshi, mtu akiwa na hatimiliki anaweza kwenda kukopa, anaweza kuweka dhamana.”

Habari Zifananazo

Back to top button