Wanaume kapimeni VVU acheni kuwategea wake zenu-Majaliwa

DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanaume kujitokeza kwenda kupima maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ili kuzijua hali zao.
Amezungumza hayo Desemba 2, 2023, wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mara baada ya kushiriki matembezi hayo kwa Km.

5 ambayo yameratibiwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT).

Majaliwa amewaomba Viongozi wa Dini kuwa mastari wa mbele kuwasisitiza watu kujua hali zao hasa wanaume ambao wamekuwa nyuma katika hilo.
“UKIMWI bado upo, ninawaomba suala hili lipewe kipaumbele wakati wa mahubiri, hotuba na mihadhara. Endeleeni kuwakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kubadili tabia hususan zile zinazochangia maambukizi.” amesema Majaliwa
“Jana ilikuwa ni maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani. Kwenye tathmini yetu, malengo ya 95-95-95 yamefanikiwa kwa maana ya 95 ya kwanza imeongezeka kwa sababu watu wengi wamejitokeza kupima. Hii inahamasisha upimaji na watu wanaojitokeza ni wengi lakini wanaopima sana ni wanawake. Wanaume hamuendi kupima.”
“Wanaume jitokezeni mkapime, msitegemee matokeo ya wake zenu. Mimi ndiye Balozi wa kuhamasisha wanaume kupima virusi vya UKIMWI, kwa hiyo msiniaibishe. Kuanzia leo, nendeni kwenye vituo vyetu mkapime VVU.”
Kuhusu 95 ya pili, Waziri Mkuu amesema hii imefanikiwa kwani waliopima na kugundulika wanatumia dawa kama inavyoshauriwa na 95 ya tatu imefanikiwa kwani wanaotumia dawa, kwa asilimia kubwa wamefanikiwa kufubaza virusi hivyo.
Amewataka viongozi hao wawaangalie zaidi vijana kwani ni kundi lililo kwenye hatari zaidi. “Kwa kuwa kundi la vijana liko katika hatari zaidi ya kupata maambukizi, ninawasihi sana imarisheni huduma za unasihi na malezi.
Advertisement

Ninayo imani kuwa, kwa nafasi zenu ndani ya jamii, vijana watawasikia, watawatii na kubadilika.”

 
2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *