Wanaume wapigwa marufuku kusuka

SERIKALI  ya Zanzibar kupitia Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni limepiga marufuku wanaume kusuka nywele kama za wasichana na atakaekiuka atatoa faini ya sh milioni 1.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Omar Adam amesema amesema kama serikali haipendelei  wanaume kusuka nywele za kike kwa kuwa sio utamaduni wao

“Askari wanakamata wanaume wote wanaosuka nywele kama za wasichana.” Amesisitiza na kuongeza

Advertisement

“Baraza la sanaa hatupendelei hilo kwa sababu sio utamaduni wetu na kuna kibali maalumu cha kusuka nywele ambacho ni Sh milioni 1,  na tumeweka bei hiyo ili kuwakomoa, sasa utachagua mwenyewe utoe sh milioni 1 usuke, au ununue kiwembe chako cha 100 unyoe.” Amesema

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *