Wanaume watakiwa kujitokeza kupinga utatili.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ,Dk Dorothy Gwajima amewahimiza wanaume kujitokeza na kushiriki kupinga ukatili wa kijinsia kwani na wenyewe wanapitia hali hiyo iwe kwa wanawake ama wao wenyewe.
Dk Gwajima amesema haya Desemba 4, 2022 mjini Morogoro, akiwa kwenye ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli zinazofanyika katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mikoa mbalimbali nchini ambazo huadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10
Amewataka watumie karama ya uongozi waliyonayo kuongoza kwa heshima badala ya kutumia misuli na matokeo yake wanakatili wanawake na watoto.
Dk Gwajima pia amezitaka kamati za ulinzi wanawake na watoto kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zilizofanyika kwenye maeneo yao katika siku 16 za kupinga ujatili wa kijinsia.
Kuhusu Ukatili katika eneo la elimu hasa shule za msingi na agizo la waajiri wa mabasi ya shule (School bus) kuwa na mtumishi moja wapo wakike amesisitiza maelekezo yameshatolewa na serikali.
” Maelekezo yameshatolewa na serikaki na kilichobaki ni maandishi tu ambayo haizuii kuanza utekelezaji wake ni jambo la dharura kwamba waajiri wenye school bus kuaji
ari mtumishi mmojawapo wa gari hizo awe mwanamke”amesema Dk Gwajima
Dk Gwajima amesema suala la ukatili limo ndani ya jamii na wenye uwezo wa kulimaliza ni jamii yenyewe kwa watu kutoa ushirikiano wa taarifa kwa serikali na yenyewe kukemea matendo maovu.