‘Wanawake changamkieni fursa kwenye ubaharia’

TAKWIMU zinaonesha idadi ya mabaharia Tanzania ni takribani 9,000,  huku wanawake wakiwa ni chini ya asilimia moja.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya Ilemela (DC), Hassan Masala, wakati akifunga maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani leo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, yaliyoratibiwa na Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC).

Kutokana na hali hiyo, akawashauri vijana wa kike kujikita katika masomo ya ubaharia, si tu kuziba pengo la ubaharia kijinsia, bali kuchangamkia fursa zilizomo katika sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji.

Amesistiza kwamba sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji ina fursa nyingi kiuchumi, kwani asilimia 90 ya biashara yote ya kimataifa duniani inabebwa na meli.

“Kwa hiyo mabaharia ndio nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa dunia na taifa kwa ujumla, kwani ndio wanaohusika kusafirisha biashara hizo,” amesema na kuongeza kuwa:

“Wakati huo huo  mabaharia ni kiungo muhimu katika kulinda mazingira kwenye maji, kama mikataba ya kimataifa iliyosainiwa na serikali ya Tanzania inavyoelekeza,  ili kulinda afya za viumbe waliomo na watumiaji wa usafiri huo.”

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button