“Wanawake msisahau majukumu yenu”

MWANZA: MTANDAO wa Polisi Wanawake wa Jeshi la Polisi (TPF-Net) Mkoa wa Mwanza umewataka wanawake wafanyabiashara wa Samaki katika Soko la Kamanga jijini Mwanza kutosahau majukumu yao ya  msingi katika familia.

Wito huo umetolewa Machi 06, 2024 na Mwenyekiti wa mtandao huo mkoani Mwanza, Mrakibu wa Polisi (SP) Virginia Sodoka, wakati wanachama wa mtandao huo walipotembelea na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake wajasiriamali kuelekea maadhimisho ya ‘Siku ya Wanawake Duniani’.

Mrakibu Sodoka ambaye pia ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana amesema tabia za wanawake wajasiriamali kujitafutia kipato ‘fedha’ na kusahau wajibu wao katika malezi ya familia kinachangia familia kusambaratika, jambo linalohatarisha usalama na kupelekea watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili.

“Hizi pesa tunatafuta kwa shida tuwe makini, pata pesa yako badili maisha ya familia yako ili familia ifurahie uwepo wako na utapata baraka” amesema.

Naye mfanyabiashara wa samaki katika soko la Kamanga Jijini humo, Veronica Charo amekiri kuwepo wajasiriamali wanaojisahau na kutelekeza familia jambo linalotengeneza mazingira hatarishi kwa Watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button