Wanawake Shinyanga wamfagilia Samia

WANAWAKE mkoani Shinyanga wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, mjini New Delhi nchini India.

Wakizungumza kwenye kongamano mjini Shinyanga, wanawake, ambalo liliongozwa na Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Christina Mndeme na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, Mabala Mlolwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed, wamempongeza pia Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo.

Advertisement

Mndeme aliwaeleza wanawake hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, imetoa fedha nyingi za maendeleo na kila kijiji kimefikiwa na mradi, ambapo sekta ya elimu serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 53.6, ambapo shule mpya 24 zimeongezeka,maabara 57 kwa shule za sekondari na nyumba za walimu 69.


Amesema upande wa nishati ya umeme, serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 323 kwa ajili ya mradi mkubwa wa nishati ya umeme jua utakuwa kwenye Kijiji cha Talagha, wilayani Kishapu ambao utakuwa ni mradi mkubwa kwa Afrika Mashariki .

Mndeme amesema kupitia mradi wa nishati ya umeme vijijini (REA) kwa mkoa wa Shinyanga vijiji 240 vimepitiwa na umeme huo, hayo ni mafanikio makubwa.

Amesema katika sekta ya afya hospitali zilikuwa nane na sasa zimeongezeka mbili na kufikia hospitali kumi , ambapo hospitali ya Halmashauri Ushetu na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga zimeanza kufanya kazi na vituo vya afya vimeongezeka sita na kufikia 25 na zahanati 11 zimeongezeka nakufikia zahanati 242.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *