Wanawake waathirika zaidi mabadiliko tabianchi

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) Afrika na Mashariki ya Kati, Dk Wassam El Beih amesema wanawake wanaathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuliko wanaume.

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni kama vile ukame, mafuriko,ongezeko la joto, ukosefu wa usalama wa chakula, kuhamishwa, vurugu na hatari za kiafya.

Akizungumza wakati akitoa mada katika mkutano wa kimaifa wa mabadiliko ya tabianchi (COP28) uliomalizika Disemba 12,2023 El Beih amesema kuna haja ya kuwepo kwa sera ambayo itasaidia utoaji wa elimu na maarifa ili wanawake waweze kutumia fursa zilizpo katika mabadiliko hayo.

“Tulijadili kwa mifano halisi jinsi mabadiliko ya tabinachi yanavyofanya wanawake na mabinti kuhama na yanavyoathiri wanawake na mabinti tofauti zaidi ya wanaume na wavulana na hiki kimejitokeza na tunataka kuhamisha maarifaa katika kutengeneza sera, program mbalimbali na kubainisha mapungufu na elimu kutolewa ili sauti za watu ziweze kusikika.

Alisema hatua ya mabadiliko itafanya wadau mbalimbali kutoka katika sekta binafsi ,asasi za kiraia,serikali na vyombo vya habari kuungana kuweka vipaumbele na kubainisha sera.

“Mapungufu yaliooneshwa na wadau katika majadiliano ya COP28 sera nyingi hazifanyi kazi na kuchukua hatua muhimu ambazo ni rafiki kwa watu kutokana na jamii na nchi bado kuna pengo pia kingine ni namna ya kustahimili kwa sera ambao zinahusiana na nchi husika na sio kuonekana tu lakini zifanye kazi kwa changamoto iliyopo katika nchi.

Alibainisha kuwa wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi ni vyema kutengeneza nafasi ya Sauti za wanawake kwani zinatakiwa kusikika na kupewa uwezo na elimu.

“IDRC tunaunga mkono tafiti zenye ubora mkubwa ambayo ina taarifa za kutosha tutaendelea kufanya kazi ya kuziba mapengo katika elimu na kuhakikisha watunga sera kuona na kufanya mabadiliko,”alisisitiza El Beih.

Mkurugenzi wa Mipango wa Kituo cha Utafiti Cha Maendeleo ya Kimataifa (IDRC) Erin Tansey alisema bado nchi za Kiafrika haziipi kipaumbele uhamiaji unatokana na mabadiliko ya tabianchi kama inavyostahili.

“Kuna haja ya kujiandaa kwa matukio kama hayo kwani athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa zinajidhihirisha katika bara la Afrika,wanawake wanalazimika kuhama lakini wanabeba majukumu mengi kama walezi wa watoto, wanaangalia wagonjwa, utunzaji wa nyumba.

Alisema mipango ya makazi mapya ni muhimu ambayo yanahitaji rasilimali, mtazamo unaozingatia jinsia, na inapaswa kuwa kwa wakati pia.

“Taasisi za utafiti zinahitaji kufanya na kushiriki matokeo kati ya washiriki wa utafiti na jamii zilizoathiriwa, kwani athari za mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na hali mbaya ya hewa, huathiri maisha, uzalishaji na usalama wa watu kote ulimwenguni, haswa jamii zilizo hatarini zaidi.

Aidha amefafanua kuwa kituo cha ufuatiliaji wa uhamisho kiligundua kuwa wastani wa watu milioni 21.5 walihamishwa kwa nguvu kutokana na majanga ya ghafla yanayohusiana na hali ya hewa kila mwaka kati ya 2008 na 2015.

Amesema Benki ya Dunia inakadiria kuwa hadi watu milioni 216 wanaweza kulazimishwa kuhama ndani ya nchi zao ifikapo 2050 ambapo hali hiyo itaibuka haraka mwaka 2030 na kuongezeka ifikapo 2050 huku nchi zinazoendelea zikiathirika zaidi .

“Karibu watu bilioni 3.3 hadi bilioni 3.6 wanaishi katika maeneo yenye joto kali ikiwa ni pamoja na Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo inachukua milioni 86 wahamiaji ni milioni 19 zaidi katika Afrika Kaskazini, na wahamiaji milioni 40 wanaotarajiwa Asia Kusini.

Image Credit: WIPO Magazine.

Habari Zifananazo

Back to top button