Wanawake wajasiriamali na njia za kupinga ukatili

DAR ES SALAAM:TAASISI ya Her Initiative inayoendesha  na jukwaa kubwa la panda digital imezindua jukwaa jipya la ongea Hub kwa kutumia ujumbe wa simu (sms) kwa wajasiriamali kuripoti rushwa za ngono.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Her Initiative, Lydia Charles amesema lengo la Panda digital ni kusaidia wasichana kupata ujuzi wa rasilimali za kuanza na kuendesha biashara zao pamoja na kupinga ukatili.

“Katika kufikia uchumi wa kidigitali, ongea Hub ni jukwaa la kiswahili linalowapa nafasi wasichana wajasiriamali kuripoti kesi za rushwa ya ngono na kuwaunganisha na mamlaka zinazotoa msaada wa kisheria, kisaikolojia, kijamii na kihisia”amesema.

Advertisement

Amesema tatizo la rushwa ya ngono kwa wasichana wajasiriamali limeendelea kuwa changamoto kubwa Tanzania, japo hakuna tafiti za moja kwa moja zinazoeleza ukubwa wa tatizo hili.

“Yapo makundi ambayo tafiti zimebainisha jinsi rushwa ya ngono imeathiri makundi, utafiti uliofanywa na Takukuru mwaka 2020 ulibaini kuwepo kwa rushwa ya ngono katika Taasisi za elimu ya juu.”

“Ikiwa imeonyesha kuwa asilimia 60 ya wanao kamatwa na matendo hayo maovu ya rushwa ya ngono ni wahadhiri wa vyuo vikuu na vyuo vya kati.”

Pia chama Cha waandishi wa habari wanawake Tanzania katika tafiti yao inaonyesha kuwa asilimia 48 ndio wanaoweza kujieleza kuhusu manyanyaso hayo ya rushwa ya ngono japo wachache hawajawa wazi juu ya kuripoti.

Ongea Hub sms ni suluhisho kwa wasichana wajasiliamali wanaopitia adha ya rushwa ya ngono lakini hawamiliki simu janja au hawana, upatikanaji mzuri wa mitandao pia hawajui msaada gani wanahitaji au wanaogopa kuwashtaki wakiofia sababu tofauti ikiwemo uoga na aibu kutoka kwa jamii.

Ilikutumia jukwaa hili tuma SMS tuma neno sajili kupitia namba 0767680463 na kwawanao miliki simu janja waweza tembelea tovuti ya www.pandadigital.com.tz na chagua Ongea hub kwenye menu kuu mfumo wa uzalishaji wa jukwaa hili ni wa siri kabisa na unaheshimu na kulinda taarifa za msichana.”amesema Lydia

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *