Wanawake, watoto wasiachwe nyuma mradi LTIP

SERIKALI imetaka wanawake na watoto wasiachwe nyuma katika kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya wilaya na vijiji inayofanyika chini ya Mradi wa Uboresha Usalama wa Milki za Ardhi nchini (LTIP).

Haya yamebainishwa Afisa Maendeleo Mwandamizi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tumaini Setumbi wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilaya ya Mufindi mkoani Njombe.

Wilaya ya Mufindi ni miongoni mwa wilaya sita ambazo zinatekeleza mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi, huku zingine zikiwa ni Chamwino, Longido, Mbinga, Maswa na Songwe.

Advertisement

Amesema, ni vyema kuwepo na ushirikishwaji wa jamii hasa makundi maalum ya wanawake, wazee, vijana na watoto hatua ambayo itaweza kujua haki zao katika kumiliki ardhi.

“Tuhakikishe wanawake, watoto wasiachwe nyuma katika vikao vya maandalizi ya mpango wa matumizi ya ardhi ya vijiji ili jamii ijue umuhimu wa kumiliki ardhi na kuongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi.”

Aidha, amesema utekelezai wa mradi huo utasaidia kuondokana na migororo ya aridhi na wananchi kutambua maeneo na matumizi yake.

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa, Katibu Tawala wa Wilaya Fank Sichalwe amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia utolewaji wa fedha zaidi ya Sh bilioni 340 kutokana Benki ya Dunia kwa ajili ya kupanga matumizi bora ya ardhi katika halmashauri sita.

Awali, diwani wa kata ya Igombavavu alisema wananchi wamefurahisha na utekelezaji wa mradi huo ambao umetenda haki.

“Mradi huu umetenda haki kwani wakati wa kupima mke na mume wote wanashirikishwa na kama ardhi hiyo ina wanandugu wanne basi kila mmoja anapimiwa kipande chake.”

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *