Wanne hawajatambuliwa ajali ya Njombe

Wanne hawajatambuliwa ajali ya Njombe

WATU watatu kati ya saba waliokufa kwenye ajali ya basi la New Force katika Kijiji cha Igando mkoani Njombe juzi, wametambuliwa na ndugu zao, wengine wanne bado.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Makuri alipozungumza na HabariLEO jana.

Kamanda Makuri alisema miongoni mwa watu hao watatu waliotambuliwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikosi cha 514 KJ Mafinga.

Advertisement

Alisema dereva wa basi hilo ni miongoni mwa watu saba waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo pia ilisababisha watu 48 kujeruhiwa.

Pia alisema majeruhi saba kati ya 48 wameruhusiwa kutoka hospitali na wengine 41 wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Ilembula mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda Makuri, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kujaribu kupita lori lililokuwa mbele yake katika eneo la daraja bila kuchukua tahadhari.

Alisema wakati dereva huyo anapita lori hilo, ghafla aliona lori jingine likija mbele yake ndipo akaamua kugonga daraja na kuangusha gari korongoni.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *