Wateka mtoto, wataka wapewe Sh Mil 50

WATU wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa  kutuhuma za kumteka binti mwenye umri wa miaka 9, kisha kumfungia ndani ya chumba kwa zaidi ya siku moja na kutishia kumuua kwa madai walipwe Sh milioni 50 ili wamuachie.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema watuhumiwa hao ni Joseph John(24) Yusuph Sadick  (27) wakazi wa Mtaa wa Milupwa, Abrahamu Kassim (28) Mkazi wa Mtaa wa Misunkumilo Manispaa ya Mpanda na Samwel Nzobe (41), Mkazi wa Mtaa wa Kotazi Manispaa ya Mpanda.

Amesema watuhumiwa hao wote wanne wamekamatwa kufuatia msako mkali ulifanywa na Jeshi la Polisi , baada ya jeshi hilo kupata tarifa ya kutekwa kwa mtoto huyo mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Mizengo Pinda iliyopo Manispaa ya Mpanda.

Kaimu Ngonyani amebainisha kuwa tukio lilitokea mnamo Juni 13, 2023 majira ya saa  nane mchana katika Manispaa ya Mpanda, wakati mtoto huyo alipokuwa akitokea shuleni, ambako alienda kufanya usafi.

Ameeleza kuwa wakati akiwa njiani maeneo ya jirani na Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kuelekea nyumbani kwao, ndipo watuhumiwa hao wanne walipomteka na kumpeleka kusikojulikana na kumtishia kumuua, hadi walipwe Sh milioni 50 ndipo waweze kumuachia.

Amesema Juni 14 walifanikiwa  kumpata mtoto huyo, akiwa salama huko katika maeneo ya Mtaa wa Milupwa Manispaa ya Mpanda,  akiwa amefichwa ndani ya chumba cha mtuhumiwa Joseph John.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button