Wanne mbaroni tuhuma za mauaji

MWANZA: Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Januari 31, 2024 na kusomewa shtaka la mauaji ya watu wawili katika kesi namba 2536 ya mwaka 2024.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo ,John Jagadi mwendesha mashtaka, mkaguzi wa Polisi Juma Kiparo amewataja kwa majina washtakiwa hao kuwa ni Michael Kanzaga ( 19), Malimi Lutema ( 42), Juma Bupilipili ( 32 ) na Kulwa Wangale ( 43 ) wote wakazi wa kijiji cha Malemve wilayani Kwimba.

Kiparo ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 11, 2024 huko wilayani Kwimba kwa kumuua Yusuph Mosha (33) mkazi wa Nyamhongoro na Galila Lutobeka (30) Dereva bodaboda na mkazi Nyamhongoro kwa kuwapiga mawe na kuwachoma moto wakiwatuhumu kwa wizi wa kuku kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka kisheria ya kusikiliza shauri hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button