Wanne wafa mto ukisomba makazi DR Congo

WATU wanne wamekufa na wengine 20 wakihofiwa kutoweka baada ya mto kusomba baadhi ya majengo huko Kivu Kusini Mashariki mwa DR Congo.

Tukio hilo limetokea eneo la Mwenga maarufu kwa shughuli za uchimbaji madini.

“Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi” kulingana na Naibu Meya wa Kamituga, mji mkuu katika eneo la Mashariki la Kivu Kusini. Mvua hizo pia zilisababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Wataalamu wanasema matukio ya hali ya hewa kali yanatokea kwa kasi na kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button