Wanufaika na kuku soko la Kisutu
WAFANYABIASHARA wa viungo mbalimbali vya kuku wanafurika katika Soko la Kuku Kisutu lililopo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma hiyo kutoka kwa wauzaji na wachinjaji wa mifugo hiyo.
Viungo hivyo ni vichwa vya kuku, miguu, firigisi, maini, utumbo, shingo, paja na kibawa.
Hayo yamebainika leo katika soko hilo baada ya HabariLeo kufika sokoni hapo na kushuhudia wanawake kwa wanaume wakisubiri kuku wachinjwe kasha wachukue viungo hivyo.
Mfanyabiashara kutoka Kigambano, Rahma Maulid amesema amefika sokoni hapo saa saba mchana huchukua saa mbili mpaka tatu ili kukamilisha mchakato huo wa kupata bidhaa aliyoifuata.
“Viungo vyote hivyo ninavinunua kw ash 200 ila utumbo wa kuku ni sh 50,” amesema.
Ameeleza kuwa baada ya kuvikaanga huuza paja sh kibawa sh 500, shingo sh 600, kichwa sh 150, firigisi na maini sh 500, kidari sh 2000 na paja sh 2000.
Amesema anashukuru biashara yake hiyo inamalizika kila siku na kwenda kuchukua mzigo mpya.