Wanufaika TASAF wafaidika na Sh bilioni 3.1

Sh bilioni 3.1 zimekopeshwa kwa wanufaika wa mpango wa kusaidia kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na tayari  fedha hizo zimeshaingia kwenye mzunguko kwa wanufaika hao wa kuanza kukopeshana na kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Afisa miradi kitengo cha kuweka na kukuza uchumi wa kaya, Anzanukye Mselela alisema hayo wakati  wa maonyesho ya sita ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi zinazofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Centre mjini Kigoma.

Advertisement

  Anzanukye Mselela afisa miradi kitengo cha kuweka na kukuza uchumi wa kaya TASAF Makao makuu

Mselela alisema kuwa fedha hizo zilizokopeshwa ni  sehemu ya kiasi cha shilingi Bilioni 7.9 ambazo kimekusanywa  kama akiba na mikopo kutoka vikundi 46,000 vilivyoanzishwa Tanzania Bara na Zanzibar fedha zinazotokana na wanufaika wa mpango wa uhaulishaji fedha TASAF kuweka hisa na amana ili waweze kukopeshana.

Afisa miradi huyo wa TASAF alisema kuwa kukopeshwa kwa fedha hizo ni sehemu ya mafanikio ya mpango wa uhaulishaji fedha kwa kaya masikini ambapo vikundi hivyo vimeundwa sambamba na kutolewa kwa elimu ya ujasiliamali kwa walengwa hao ambapo miradi mbalimbali imeanzishwa.

Pendo Weja Mnufaika wa TASAF Kutoka Tabora anayeshiriki maonyesho ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika mjini Kigoma

Hali hiyo alisema kuwa inatoa unafuu kwa wanufaika hao kukua na kumaliza muda wao wa kupata malipo kwenye mfuko huo wakiwa na uwezo wa kujihudumia tofauti na maisha waliyokuwa nayo awali kabla ya kuanza kusaidiwa na mfuko huo.

Baadhi ya walengwa wa mpango huo ambao wamenufaika na fedha za uhaulishaji kutoka TASAF akiwemo Pendo Weja kutoka mkoani Tabora alisema kuwa wakati wanapokea fedha zinazotolewa kwenye mpango huo alikuwa wakitumia kwa shughuli zilizopangwa kwa ruzuku za masharti na fedha kidogo wakawa wanaweka ili wazitumie kama mtaji.

Asia Jaffari Mnufaika wa TASAF kutoka Urambo mkoani Tabora

Naye Asia Jaffari mnufaika wa TASAF kutoka mkoani Tabora ambaye anashiriki maoenyesho ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika mjini Kigoma alisema kuwa vikundi vya akiba na mikopo walivyoanzishwa walengwa wa TASAF vimekuwa na mafanikio makubwa kwao kwa kuweza kuweka akiba na kukopeshana fedha ambazo wamezitumia kuanzisha miradi ya kiuchumi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *