Wanufaika wa mikopo waipongeza serikali

WAJASIRIAMALI katika Jiji la Dodoma walionufaika na mikopo ya Sh milioni 170 iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu wameipongeza serikali kwa kuwajali kwani imesaidia katika kuinua maisha yao.

Wajasiriamali hao walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Zainab Chaula.

Mkurugenzi wa kampuni inayojishughulisha na uchakataji wa taka za plastiki, Aziza Abdi ambaye alipokea mkopo wa Sh milioni 100 alisema ameweza kupanua biashara yake ambapo kwa sasa ana uwezo wa kuchakata tani 130 kwa mwezi tofauti na hapo awali walipoanza mwaka 2013 ambapo walikuwa wakichakata tani 40 pekee.

“Mbali na kuongeza uzalishaji, lakini kwa sasa nimenunua gari moja na kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 20 hadi 60 wa kudumu sambamba na kuboresha maslahi yao,” alisema.

Yolanda Kaswalala anayejishughulisha na uchakataji wa bidhaa za mafuta ukiwepo uzalishaji wa mafuta ya alizeti, usagaji unga na ukoboaji wa nafaka ambaye alipata mkopo wa Sh milioni 50, aliipongeza serikali kwani ameongeza mashine zaidi.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Dk Chaula alisema: “Ziara yetu hii ni ya kuamsha ari na kuchochea morali kwa wanajamii wenyewe watumie rasilimali zinazowazunguka ili waweze kuzibadilisha changamoto kuwa fursa.”

Alisema umefika utafiti na wanaokidhi vigezo wapatiwe alama za ubora.wakati kwa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa ndani kufanyiwa

Habari Zifananazo

Back to top button