Waomba utatuzi changamoto za mtoto wa kike

Waomba utatuzi changamoto za mtoto wa kike

WATOTO wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini,  wameiomba serikali kuhakikisha inaondoa mifumo yote ya kisheria inayokwamisha upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike, hasa anayeishi kijijini

Akizungumza Dar es Salaam katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike, mwanafunzi wa Mkoa Tabora, Loveness Athuman, amesema siku hiyo inalenga kutatua changamoto za mtoto wa kike na kumpa mwanga.

Amesema mtoto wa kike aachwe asome,  ili kufikia ndoto zake na sio kuolewa.

Advertisement

Pia wameiomba serikali, iangalie marekebisho ya sheria ya ndoa na bei za taulo za kike zipunguzwe.

Kongamano hilo lililoandaliwa na mashirika na taasisi mbalimbali nchini, ikiwemo Girl Agenda, Msichana Iniviative Organisation, UNFPA, Flaviana Matata,  Girl Effect na UN Women