KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi amesema serikali itamchukulia hatua mwongoza utalii atakayegundulika kusababisha watalii kuondoka nchini kwa kutowapa huduma nzuri zilizopo katika sekta hiyo muhimu nchini.
Dk, Abbasi ameyasema hayo leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne ya waongoza utalii zaidi ya 1,032 yaliyotolewa na Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA).
Amesema uongo katika sekta ya utalii hautakubalika na endapo itabainika waongoza utalii wanasababisha watalii kuondoka nchini Tanzania serikali itachukulia hatua
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),William Mwakilema amesema Tanapa imejipanga kutangaza hifadhi tano ikiwemo Hifadhi ya Mkomazi ambayo awali zilikuwa hazitangazwi sana katika sekta hiyo ya Utalii
Alizitaja hifadhi nyingine ambazo ni Saadani,Mikumi, Nyerere na Ruaha ambazo zimekuwa hazijulikani sana hivyo Tanapa imedhamiria kuzitangaza zaidi na kuziweka kwenye vifurushi vya safari za waongoza utalii nchini
Amesema utaratibu wa kufanya utalii katika vivuko vya nyumbu nakuazimia kwa pamoja waongoza utalii kuzingatia sheria na kanuni ikiwemo usafi wa mazingira kwa kwakushirikiana Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Tanapa na wadau mbalimbali wataandaa vipeperushi maalum vya kutunza mazingira.
Naye Mwakilishi wa Waongoza Watalii Tanzania,Ridas Mollel semina hiyo iliyoshirikisha waongoza utalii zaidi ya 1,302 ni chachu ya kuongeza idadi ya watalii milioni 5 ifikapo 2025 ambapo pia waliomba waongoza watalii hao kupata mikataba ya kazi ikiwemo viwango maalum vya malipo.