Waonywa matumizi ya kinga zilizoisha muda

MTAALAMU wa uchunguzi vifaa tiba katika Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) Jovin George amesema utumiaji wa kinga zilizoisha muda wake katika tendo la ndoa unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya mtumia kutokana na viwango vya ubora kupungua.

Akizungumza na HabariLEO katika mahojiano maalum mtaalamu huyo amesema miongoni mwa madhara ni kuambukizwa magonjwa ya zinaa na maabukizi ya virusi vya Ukimwi.

“Madhara ambayo anapata mtu ambaye kondom yake inaisha muda ni kondom inaweza kuwa na matobo au matundu na vilevile inaweza kushindwa kustahimili misuguano kutokana na kutokuwa na ubora na hali hiyo inaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa,”amesisitiza.

Advertisement

Aidha amewashauri watumiaji wanapoenda kununua kondom waangalie muda wa matumizi kuisha ili waweze kutumia bidhaa iliyo na ubora na usalama.

Amesema Kwenye kondom wanapima vitu mbalimbali kama vile ukubwa,unene ,urefu na wembamba wa kondom lakini vilevile wanaangali uimara na kama inamatobo.

“Kuna miongozo ambayo inatuelekeza kama kwa kila toleo ni ngapi upime na ngapi zikifaulu ndo iwe salama kwamfano kwenye hili toleo tunapima uimara ya 315 haitakiwi iwe chini ya hapo kwa kondom pisi 10 na kuendelea maana yake imefeli.

Ameeleza kuwa hatua ya kwanza ni kuamua nini anapima?

kama ni matobo ,uimara,urefu,upana na unene na anaangalia viwango vinasemaje ambapo kwa urefu wanapima pisi 13 iwe na sentimeta 160 kwenda juu ikiwa chini ya hapo haina viwango vinavyotakiwa na kama ni unene pia unaangalia maelekezo ya utengenezaji.

“Upana wa kondo kwa kawaida ni mill 53 kwa nyingi na kulingana na viwango vya utengenezaji iwe hapo hapo,”amesisitiza.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *