WAKAZI wa Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuacha tabia ya uharibifu wa miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Meneja wa shirika hilo mkoani hapa, Said Msemo amesema hayo wakati wa mahojiano maalum na mtandao wa HabariLEO.
Amesema mpaka sasa ni zaidi ya wateja wao 150 wameathirika na ubadhirifu wa miundombinu na kulipa hasara shirika hilo zaidi ya Sh milioni 151.
“hivi karibuni Kumeibuka changamoto ya wizi, ubadhirifu na uharibigu wa miundo mbinu ya Umeme na kulipa Shirika hasara Kwa kuiba,kuangusha na kuchukua mafuta ya Transfoma.” amesema Msemo.
Ameweka wazi kuwa kuanzia mwezi Machi mpaka Juni mwaka huu shirika hilo limeishapoteza transfoma sita katika Wilaya za Magu, Kwimba na Misungwi.
Amesema upotevu wa transfoma hizo umesababisha baadhi ya wateja kukosa huduma hiyo na kusababisha Shirika hilo kukosa mapato ya Sh milioni 9 kwa siku.
“Thamani ya Transfoma hizi zilizoibiwa peke yake ni zaidi ya Sh milioni 51 na kama shirika ukiachilia mbali changamoto walizozipata hawa wateja 150 tumeweza kukosa mapato ya milioni 9 Kwa siku kwahyo ukijumlisha Transfoma na mapato haya ambayo tumekosa tumepoteza zaidi ya milioni 60.” amesema Msemo
Amesema kuwa mpaka Sasa wanawashukiwa wanne wanaodhaniwa kuwa wameshiriki ubadhirifu huo huku wengine wakiendelea kusakwa. Msemo ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa shirika hilo kwa kulinda miundo mbinu hiyo.