Wapalestina wengine 18 wauawa

TAKRIBAN Wapalestina 18 wameuawa baada ya mashambulizi ya Israel kulenga nyumba moja huko Khan Younis usiku kuamkia leo. Mtandao wa Al-Jazeera unaripoti.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu anasema Gaza imekuwa sehemu mbaya yenye kukata tamaa kwa maisha ya Wapalestina.

Lebanon iliwasilisha malalamiko rasmi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikisema kuwa Israel ilirusha makombora sita katika shambulio lililomuua naibu kiongozi wa Hamas Saleh al-Arouri katika kitongoji cha Beirut.

Takriban watu 22,600 waliuawa na 57,910 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza tangu Oktoba 7.

Habari Zifananazo

Back to top button