Wapandishwa vyeo kuwa wakaguzi wasaidizi wa polisi

ARUSHA: MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IJP), Camillus Wambura leo Januari 02, 2024 amewapandisha vyeo Konstebo wa Polisi Hussein Mwalubebe na Richard Msesi wa kikosi cha kutuliza ghasia Mkoa wa Arusha na kuwa Wakaguzi wasaidizi wa polisi nakuvishwa vyeo hivyo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi.

ACP Masejo amesema kuwa askari hao wamepandishwa cheo hicho kutokana na sifa na utendaji bora wa kazi za Jeshi la Polisi.

Aidha,Kamanda Masejo amewataka wakaguzi hao kutambua nafasi ya cheo walichopata kuwa ni dhamana ya kuaminiwa na Mkuu wa Jeshi ambapo amewataka kusimamia vyema askari walio chini yao ili kupunguza malalamiko ya wananchi.

Habari Zifananazo

Back to top button