Wapeleka migogoro ya ndoa Takukuru

Wapeleka migogoro ya ndoa Takukuru

MIGOGORO ya ndoa ni sehemu ya malalamiko mengi yasiyohusiana na rushwa yaliyoelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Iringa kuwasilishwa kwao.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba, mwaka jana; Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Domina Mukama aliitaja migorogoro mingine kuwa ni ile inayohusiana na mirathi na ardhi.

“Taarifa zisizohusu rushwa zimekuwa nyingi kuliko zinahusu rushwa kwa sababu wananchi wengi wana imani kwamba Takukuru inaweza kusaidia ishughulikiwe kwa haraka,” alisema.

Advertisement

Alisema katika robo hiyo ya mwaka walipokea malalamiko 44 ambayo kati yake 24 yalihusu migogoro hiyo na 20 yaliyobaki ndiyo yaliyoangukia kwenye rushwa.

“Taarifa 24 ambazo hazikuhusu rushwa zimeshughulikiwa kwa njia ya uelimishaji, uzuiaji na ushauri na 20 zinazohusu rushwa zimeshughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kuanzisha uchunguzi,” alisema.