Wapeni ruhusa wafanyakazi wakamuage Mzee Rukhsa

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ametoa wito kwa watumishi wa serikali, wafanyakazi na wanafunzi kupewa nafasi ya kwenda uwanja wa Uhuru kuuaga mwili wa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Chalamila amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, wanafunzi wote wa shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu waruhusiwe mara moja kuwa sehemu ya watakaouaga mwili huo.

Chalamila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Dar es Salaam, amesema vyombo vya ulinzi vipo imara katika kuhakikisha wote watakuofika uwanja wa Uhuru au hata barabarani wanaaaga za kurudi salama.

Advertisement

“Niwahakikishie kwamba vyombo vyote ya ulinzi viko salama, na wala mtu yoyote asiogope au kusita kuhudhuria msiba huu mkubwa ili tutoe heshima za mwisho”.amesema Chalamila.