Wapewa mbinu ukusanyaji mapato Mtwara Mikindani

Wapewa mbinu ukusanyaji mapato Mtwara Mikindani

MEYA wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Shadida Ndile amewataka watendaji wa manispaa hiyo kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wananchi, ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.

Amesema hatua hiyo itasaidia wananchi kuhamasika kulipia tozo na kodi ambazo zinatakiwa kulipwa kwa hiari.

Ndile amesema hayo leo Januari 31, 2023 katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Mtwara Mikindani.

Advertisement

Amesema kumekuwepo na ukusanyaji wa mapato yasiyoridhisha, kitendo ambacho kitazorotesha jitihada za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema halmashauri hiyo kwa kiasi kikubwa inategemea uzalishaji wa zao la korosho, ambapo pia uzalishaji wake ulishuka Kwa mwaka 2022/2023.

Hata hivyo Meya huyo amesema halmashauri imeendelea kubuni miradi mbalimbali ya kimkakati, ili kuongeza ukusanyaji wa mapato huku akitaka watendaji kuongeza jitihada ili kufikia malengo hayo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *